Historia Fupi Ya Shule ya Sekondari Itilima

Shule ya sekondari Itilima ni Shule ya serikali inayopokea wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Shule ni ya bweni kwa kidato cha tano na sita ambao ni wasichana tu na kutwa kidato cha kwanza hadi cha nne ambao ni mchanganyiko (wasichana na wavulana).

Shule hii ipo katika mkoa Simiyu wilaya ya Itilima kaskazini-Magharibi mwa Tanzania.  Ni umbali wa kilometa 125 kutoka shinyanga mjini sawa na mwendo wa masaa mawili. Pia ni umbali wa kilometa 15 kutoka bariadi mjini sawa na mwendo wa nusu saa.

Shule ya Sekondari Itilima Ilianzishwa mwaka Januari, 1998 kwa upande wa kidato cha kwanza hadi cha nne na 2016 kwa kidato cha Tano na Sita.

Masomo yanayofundishwa kwa kidato cha kwanza Hadi cha nne ni Biolojia, Kemia, Historia, Uraia, Hisabati, Jeografia, Kingereza, Kiswahili, Kilimo,Litrature, Historia

Michepuo inayofundishwa kwa kidato cha Tano na Sita ni PCM, PCB, HGK,HGL