














Shule ya sekondari Itilima ilianzishwa Januari, 1998 Kwa Usajiri namba S.789 ikiwa na Jumla ya wanafunzi 80, wasichana 40 na wavulana 40. Kwasasa Inajumla wanafunzi takribani 800 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. kuna michepuo ya sayansi na sanaa kwa kidato cha tano na sita kama PCM, PCB, HGK na HGL
Shule Hii ni ya serikali iliyopo Mkoa wa Simiyu wilaya ya Itilima kata ya Luguru kaskazin-magharibi mwa Tanzania, Ni sawa na kilometa 12 kutoka bariadi mjini au mwendo wa nusu saa kwa pikipiki. Au ni mwendo wa masa 2 kutoka Shinyanga mjini sawa na umbali wa kilometa 125
Shule hii ni ya bweni kwa kidato cha tano na sita na kutwa kwa kidato cha kwanza hadi cha nne. Kwa kidato cha tano na sita ni wasichana na kwa kidato cha kwanza hadi cha nne ni mchanganyiko (wavulana na wasichana)