Habari za hivi sasa

Mtihani wa Taifa kwa kidato cha pili 2025

Kidato cha pili wanatarajia kuanza mtihani wao wa Taifa wa kumaliza kidato cha pili utakaoanza tarehe 10.Nov.2025. Tazama hapa ratiba ya mtihani kwa kidato cha pili

Mtihani wa Taifa kidato cha nne 2025

Kidato cha nne wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa ya kumaliza kidato cha nne itakayoanza tarehe 17.11.2025 . Tazama hapa ratiba ya mtihani wa kidato cha nne

Viongozi wapya Shule ya sekondari Itilima wakiapishwa na makamu mkuu wa shule waliochaguliwa kutokana na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi uliofanyika siku ya ijumaa tarehe 9.10.2025

Mitihani ya muhula kwa kidato cha tano 2025

Wanafunzi kidato cha Tano wakiwa kwenye mitihani Yao ya muhula iliyoanza J.tatu tarehe 17.11.2025

KUHUSU ITILIMA SECONDARY

Shule Ya Sekondari Itilima Ilianzishwa januari,1998 Kwa Usajili namba S.789.

Itilima sekondari inapatikana katika mkoa wa Simiyu wilaya ya Itilima Kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Ni kilometa 15 kutoka bariadi mjini sawa na mwendo wa nusu saa kwa boda au daladala

Ni kilometa 125 kutoka Shinyanga mjini(ambapo ni mwendo wa masaa 2 kwa gari)